Konki Master yaweza kua BRAND ,AY amshauri Dudu Baya kusajili ‘Konki Master’

Msanii wa muziki wa hip hop, AY amemshauri rapa Dudu Baya kusajili jina Konki Master kwani kuna baadhi ya wafanyabishara wanalinyapia.
Dudu aka Konki Master alijipatia umaarufu pitia sakata lake la kutoa list za watu wanadaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.
“Dudu Baya akitaka kutisha akasajili slogan yake akidelay si mnawajua kampuni zetu za mawasiliano kwa kudandia misemo..PATA OFFER KONKI. Mfikishieni ujumbe wangu,” alitweet AY.
Kwa sasa mkali huyo wa hit ‘Nakupenda Mpenzi’ amepata shavu la kufanya show kupitia tamasha la Wasafi Festival ambalo litazunguka katika mikoa 5.
Credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment