Mahakama yatoa hukumu kesi ya Nondo

Mahakama ya Mkoa wa Iringa imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia dhidi ya makosa yake mawili aliyokuwa akishtakiwa.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo.
Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili moja la kutoa taarifa za uongo kwa kudanganya kama alitekwa akiwa jijini Dar es salaam na baadaye kukutwa Mkoani Iringa.
Nondo alikuwa akitetewa na Wakili wa Jebra Kambole kwa kushirikiana na mawakili kutoka kituo cha Haki za binadamu na mtandao wake wanafunzi ambapo katika uamuzi huo  mahakama ilimkuta Nondo hana hatia na kuamuru aachiwe huru.
Hivi karibuni Abdull Nondo ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini aliandika barua ya kuomba kujiuzulu nafasi yake kutokana na sababu binafsi jambo ambalo  lilikubaliwa na viongozi wa mtandao huo.
Aidha Nondo pia ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakichunguzwa uraia wao na mamlaka ya uhamiaji nchini ambapo alitakiwa kuambatanisha baadhi ya Nyaraka za wazazi wake.
credit::EATV
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment