BURUDANI :: Fiesta Inakuja Dar Mwaka huu,Suprise kibao

Uongozi wa Clouds Media Group, umetangaza kuwa tamasha la Fiesta ambalo liliahirishwa kufanyika Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi Oktoba, litarudiwa tena mwezi huu.

Taarifa hizo za kurudiwa kwa tamasha hilo, zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga kupitia kipindi cha Clouds 360.
Kwa upande mwingine, bado haijaelezwa ni sehemu gani tamasha hilo litafanyika? na kiingilio kitakuwa ni shilingi ngapi?.
Tarehe 24 Oktoba mwaka huu, ni siku ambayo tamasha la Tigo Fiesta lilipangwa kufanyika, lakini baadae liliahirishwa kwa amri ya Serikali ya Manispaa ya Kinondoni.

credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment