Elimu :: Jinsi ya kununua App kutoka Google Play Store bila kutumia akaunti ya Benki

Kutoka Bongo 5 nikasema hii article niweze ku share na nyie sababu ni elimu kila mtu anahitaji kua nayo na ina manufaa mengi.
Kwa sasa Watanzania ambao wanapenda kununua programu za simu (Apps) za Android kutoka Play Store, hawatapata tabu tena ya kufanya malipo baada ya mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom Tanzania kuzindua huduma ya kulipia kwa njia ya vocha (muda wa maongezi).

Mfumo huu utasaidia mteja kufanya manunuzi ya Apps kwa njia ya  simu za mkononi, bila kulazimika kutumia malipo ya benki ambayo yana mchakato mrefu kidogo na muda mwingine sio salama katika ulinzi wa akaunti yako.
Hatua hiyo, imekuja baada ya Mtandao pendwa wa simu za mkononi nchini Tanzania wa Vodacom, kuingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Google ambayo inamiliki duka la mtandaoni la ‘Play Store’.
Kuanzia sasa wateja wenye vifaa au simu za ambao walikuwa wanatumia huduma za kibenki katika kununua programu mbalimbali za simu kupitia Google Play Store, wataweza kununua Apps kwa kutumia simu zao moja kwa moja.
Hatua hiyo iliyopigwa na Vodacom ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha na kuimarisha mfumo jumuishi  wa kifedha ambao unaziunganisha taasisi za fedha na watoa huduma mbalimbali duniani na kuondokana mfumo wa zamani wa kubeba fedha mfukoni au kwenda benki moja kwa moja.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment