Hizi ndizo Body Spray alizokuja nazo Mwana FA na Sababu kwanini kaja nazo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mumbe wa kamati katika baraza la sanaa taifa (BASATA) Mwana Fa, ameamua kuanzisha bidhaa yake ya perfume (Body Spray) aliyoipa jina la ‘FYN by FALSAFA’.


Kupitia ukurasa wake wa Instgram msanii huyo amefunguka mengi ikiwa pia sababu iliyopelekea kuanzisha bidhaa hii ambayo ameungana na baadhi ya wasanii waliofanikiwa kuanzisha kitu chao.
Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Alikiba ambaye alianzisha Tshirt za King Kiba pamoja na kofia lakini pia akaanzisha kinywaji chake kinachojulikana kama Mofaya, mwingine ni Diamond Platnumz ambaye ameanzisha vitu vingi sana ikiwemo Tv, Radio,lebo ya muziki,Karanga,Perfume na vingineo vingi, pia Mwana Fa ameungana na wasanii hawa na wengine kuwa katika rodha ya wasanii wanaomiliki bidhaa zao.

Hiki ndicho alichokieleza Mwana Fa:- ” Since wameamua kunifurahisha kwa kumfukuza Mreno,na mi nimeona tujifurahishe tu wenyewe pia na sisi,tunukie tu vizuri..kwani kitu gani bwana ๐Ÿ˜€
Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays zetu hizi hapa @FYNbyFalsafa; blue ya kiume na pink ya kike… imagine bei ya jumla ni TZS 4,000 kwa moja, SHANGAA WEWE, na niamini zitafanya unukie vizuri SANA…๐Ÿ˜€
Kuanzia wiki ijayo mzigo utakuwa madukani. Yeyote anayetaka kufanya pre-order ama kuwa msambazaji wasiliana nasi kwa namba +255766170270 au email management@mwanafa.com; nawashukuru kabisa. ๐Ÿ™๐Ÿฝ
| Smell FYN | Be FYN | #FYNbyFalsafa |”
Uwezekano Upo... Kila Wakati...
Ndoto Zinaweza Tu Kutimia Tukizikazania. Nawashukuru Kwa Support Na Naamini Tutafanya Vizuri Na Hii. Asanteni Sana.
____
Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays zetu hizi hapa @FYNbyFalsafa; BLUE ya kiume na PINK ya kike... imagine bei ya jumla ni TZS 4,000 kwa moja, SHANGAA WEWE, na niamini zitafanya unukie vizuri SANA...๐Ÿ˜€
____
Kuanzia wiki ijayo mzigo utakuwa madukani. Yeyote anayetaka kufanya pre-order ama kuwa msambazaji wasiliana nasi kwa namba +255766170270 au email management@mwanafa.com; nawashukuru kabisa. ๐Ÿ™๐Ÿฝ
____
| Smell FYN | Be FYN | #FYNbyFalsafa
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment