Ruge Ndiye ‘mkombozi wa BongoFleva’ ??Sifa 5 za Tajwa kuthibitisha

Article kutoka Bongo 5 imenivutia,soma nipe maoni yake 

Ruge alianza kujulikana rasmi kwenye tasnia ya burudani baada ya kuanza kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, na baadaye kwenye Tamasha kubwa la muziki la Fiesta, Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania THT, Semina za Fursa pamoja na mambo mengine mengi ambayo ameyafanya nyuma ya pazia. Haya ni mambo 5 ambayo ameyafanya Ruge na kuchangia ukuaji wa Mukizi wa BongoFleva Tanzania.
1. RUGE AMETENGENEZA MFUMO WA MUZIKI TANZANIA.
Huyu ni mmoja kati ya watu muhimu kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, amefungua njia kwa wasanii wengi, amesaidia kujenga mifumo ya muziki pamoja na mazingira rafiki kwa ukuaji wa muziki wa BongoFleva. Kupitia Tamasha la Fiesta ambalo ndio kubwa kwa sasa nchini Tanzania, alitoa fursa kwa wasanii kuonyesha uwezo wao, alionyesha kitu tofauti katika maandalizi ya show zake kuanzia perfomance za wasanii, light, stage pamoja na mambo mengine mengi. Mafanikio ya tamasha hilo bila shaka ndio matunda ya matamasha mengine mengi yaliozaliwa miaka hii.
Pia Ruge aliweza kuwatengeneza vijana wengi na kuwaingiza katika biashara ya muziki. Alimtoa Babu Tale katika shughuli zake na kumuingiza kwenye tasnia ya muziki, na leo hii Tale ni mmoja kati ya mameneja wanao msimamia msanii Diamond Platnumz ambaye anamiliki label ya WCB.
………………..MANENO YA BABU TALE……………………..
“Mimi nilikua nafanya kazi kwenye kampuni ya miito ya simu na nilikua nalipwa milioni 1 kwa mwezi na kwa kuwa sina elimu basi niliona kama dodo mperani. But huyu bwana (Ruge) alikuja akaniuliza hivi unazani unafanana na hii pesa unayolipwa?. Mi nikahisi ananionea gere, basi alinikazia mwezi mzima na kuniambia rudi mtaani kasaidie mtaa na pesa utapata uko zaidi ya hii nikambishia then akajitolea kuwa atakua ananipa pesa bila hata ya kumfanyia kazi but nirudi kitaani hapo nikakubali nikaingia mtaani nikakomaa mpaka leo nimepata tobo naendesha maisha yangu na timu ya masela kibao wanaenda chooni kwa ajili yangu. Mungu akuweke boss leo umezaliwa na sina zawadi ya kukupa zaidi ya madua. Happy birthday Ruge”
Ruge amekuwa akitajwa na baadhi ya wadau kwamba yeye ndiye alimfungulia njia Diamond Platnumz mpaka kupatikana kwa kolabo ya Number One na Davido.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment