Askofu Kakobe aja juu Asema ‘sipo CCM wala Chadema, nikiteuliwa na Rais nitakataa’

Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, amechukizwa na kitendo kilichofanywa na baadhi ya wanasiasa wanaosemakuwa kiongozi huyo ameigeuka CHADEMA.

Askofu kakobe amesema maneno mengi yamekuja baada ya yeye kuhudhuria kikao kati ya viongozi wa dini na Rais Dkt. John Magufuli kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Askofu Kakobe ameyasema hayo jana Jumapili Januari 27, 2019 wakati wa ibada iliyofanyika kwenye kanisa lake jijini Dar es Salaam, na kuwataka wanasiasa wote wanaomdhihaki watubu la sivyo “wataanguka kwenye shimo refu na hawatainuka tena”.
Viongozi wa siasa ambao wamewatukana viongozi wa dini kwenye mitandao ya kijamii, wanapaswa kutubu haraka sana, wakikaidi agizo hilo, chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu ambao hakitainuka tena,” aamesema Kakobe.
Kuwatukana viongozi wa dini kwa sababu hawakuzungumza yale mliyotaka kuyasikia, ni utovu wa nidhamu, ni kiburi.“.
Askofu Kakobe amedai kuwa, baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Rais Magufuli na viongozi wa dini, kuna baadhi ya viongozi wa siasa, waliwatukana viongozi wa dini kupitia mitandao ya kijamii.
Kuhusu uanachama wa CHADEMA, Askofu Kakobe amesema kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini, ingawa amekuwa akialikwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na vyama vya kisiasa.
Sijawahi kuwa mwanachama wa Chadema wala CCM..sina kadi ya vyama hivyo, sijawahi kuwasiliana na kiongozi yeyote wa Chadema wala kuonana nao ana kwa ana.“amesema Kakobe.
Kakobe aliendelea kusisitiza “Wala (CHADEMA) hawajawahi kuja ofisini kwangu, halijawahi kutokea. Naendelea kusisitiza kuwa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship halijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Hata Mbunge wa Jimbo ambalo Kanisa hili lipo, (Saed Kubenea – Chadema) sijawahi kuonana naye wala kuzungumza naye.“.

“Leo (jana) ninanena waziwazi, kanisa langu siyo Chadema wala CCM, wala chama kinginge chochote, lakini waumi wake ni wanachama wa vyama hivyo vya siasa,” amesema Askofu Kakobe
Kwa upande mwingine, Askofu Kakobe amedai kuwa hata Rais Magufuli akimteua kushika nafasi ya uongozi ndani ya nchi, hawezi kukubali kwa kuwa ana kazi maalum ya kumtumikia Mungu
Siwezi kuwa mbunge wala waziri, na hata siku ikitokea nimeteuliwa na Rais, nitasema asante, lakini sitakubali,” alisisitiza.
Waumini wangu si mnajua nina pesa, si mnafahamu nilisema mimi ni tajiri kuliko serikali, si TRA wanajua walikuta fedha nzuri tu benki, si walikuta akiba nzuri katika akaunti ya kanisa, utaninunua kwa bei gani? Sina bei mimi,” alimaliza Askofu Kakobe .
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.