Elimu:: Yajue Mashart mapya kwenye mtandao pendwa wa WhatsApp

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umenuia kuweka ukomo wa utumaji ujumbe kwa wanachama wake na sasa si zaidi ya mara tano, kwa lengo la kukabiliana na kuenea kwa habari za uongo kwenye jukwaa lake.
Wakati whatsApp wakichukua hatua hiyo, tayari mtandao mwingine wa kijamii wa Facebook tayari ulikwisha anzisha sera kama hiyo yapata miezi sita iliyopita huko nchini India .
Kwa mujibu wa BBC, Hatua hiyo inafuatia idadi kubwa ya magenge ambayo yanatumia majukwaa hayo kusambaza taarifa zisizo sahihi kwa jamii, mpaka sasa, watumiaji wa mitandao hiyo mahali kwingineko ulimwenguni, wanaweza kuchukua ujumbe na kuutuma kwa mwingine zaidi ya mara ishirini.
Usasishaji wa programu tumizi na sheria mpya ulitangazwa katika sherehe fupi mjini Jakarta, nchini Indonesia. Inaarifiwa pia kuwa nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mwezi wa nne mwaka huu.
Kampuni ya Facebook iliiambia BBC ya kwamba imefanya maamuzi hayo baada ya uchunguzi makini na kupata matokeo ya uchunguzi iliyoufanya kwa muda wa nusu mwaka nchini humo.
Mtindo wa kutumiana ujumbe uliosinyazwa una lengo la kupunguza jumbe za kutumiana baada ya kuupata kutoka sehemu ingine duniani kote, amearifu msemaji wa kampuni hiyo.
Hali hiyo ama umuzi huo utausaidia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kumakinika zaidi na jumbe binafsi na mawasiliano ya karibu. Tutaendelea kusikiliza maoni ya mtumiaji kuhusu uzoefu wake, na baada ya muda, tutaangalia njia mpya za kushughulikia maudhui na virusi. “
Kizuizi hicho kimekuja wakati WhatsApp na huduma nyingine za Facebook ziko chini ya uchunguzi kutokana na wajibu wao katika kueneza propaganda na taarifa zisizo na ukweli kwenye mitandaoni yao.
Wiki iliyopita, mtandao wa kijamii wa Facebook ulitangaza kuondoa kurasa mia tano pamoja na akaunti za watu wanaodaiwa kuhusika katika habari zisizo na ukweli Ulaya ya kati, Ukraine na nchi nyingine za mataifa ya Ulaya ya Mashariki .
Siku za karibuni pia mtandao huo ulitangaza kuanzisha kitengo kitakachotoa huduma ya kufuatilia usahihi wa taarifa na maudhui katika majukwaa yake.
Hata hivyo, matumizi ya usimbaji fiche baina ya watu wawili kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp jumbe zake zinaweza tu kusomwa kwa baina ya mtumaji na mpokeaji, ili kuendelea kupunguza uwezo wa jumbe hizo kusambaa kwingineko na hivyo kudhibiti taarifa za uongo kutosambaa
Ingawa mwishoni mwa mwaka uliopita, vyombo vya habari vya nchini India vililiripoti kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikizingatia mabadiliko Facebook na WhatsApp katika udhibiti wa maudhui. Ingawa mabadiliko hayo yametajwa kuwa ni changamoto katika matumizi ya teknolojia ya usimbaji fiche..
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.