HAMISA Mobetto'' Sijaiba Bwana wa Mtu Alikuja MWENYEWE na Ninampenda..Nifanyaje Sasa"

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto ambaye Wiki iliyopita aliingia kwenye headlines Baada ya kudaiwa kuiba bwana wa mrembo aitwaye Tahiya.


Tahiya ambaye ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond, alimtuhumu Mobetto kwa kumchukulia bwana ake anayeitwa Alex ambaye anatajwa kuwa mtoto wa Kigogo mmmoja hapa nchini.
 Hamisa Akiwa na Alex Kulia: Tahiya Akiwa na Alex


Tahiya  aliposti picha ya Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya; “Hamisa Mobeto achana na wanaume za watu.”

Baada ya muda mwanadada huyo akaposti tena meseji zao zote alizokuwa wakijibizana na mwanamitindo huyo kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo Tahiya alionekana akimsihi Mobeto aachane na mpenzi wake lakini haikusaidia kwani mwisho wa waliishia kujibizana maneno mabaya huku kila mmoja akijiona anaweza zaidi ya mwenzake.

Baada ya skendo hiyo kutawala mitandao ya kijamii Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Hamisa Mobetto ili kupata Ukweli kwa upande Wake ambapo alifunguka na kusema:
"Mnataka niwaambie nini, mlichokiona ndiyo hichohicho isitoshe mimi siyo mtoto mdogo kwa hiyo naelewa ninachokifanya, sijaiba mwanaume wa mtu ila alikuja mwenyewe na nampenda nifanyeje sasa”.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.