MAPATO:: Jiji la Dodoma laongoza kwa ukusanyaji mapato nchini

Jiji jipya la Dodoma limeongoza kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali nchini kati ya majiji 6, huku jiji la Tanga likishika mkia.
aziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ambapo aliwaagiza wakuu wa mikoa yenye halmashauri 21 ambazo zimefanya vibaya wajitathmini.
Makusanyo ya jumla yanaonyesha kuwa halmashauri zote zimekusanya 41% katika kipindi cha nusu ya mwaka, ambazo ni sawa na Tsh bilioni 300 kati ya Tsh Bilioni 735.6 zilizotarajiwa.
Waziri Jafo amewataka wakuu hao kuwasilisha maelezo yao Tamisemi juu ya sababu za kushindwa kufikia malengo na waeleze mikakati ya kuongeza mapato kwenye mikoa yao.
Katika ripoti hiyo, Jafo amesema Dodoma imekuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kufikia Tsh Bilioni 40.1 sawa na 59% ya lengo la Tsh Bilioni 68.64 ya makisio kwa mwaka 2018/19, katika kipindi cha kwanza cha mwaka wa fedha wa 2018/19 ambacho kilianzia Julai 2018 hadi Desemba 2018.
Katika kipindi hicho, Jiji la Tanga limeshika mkia kwenye orodha ya majiji sita nchini kwa kukusanya 33% ya makisio.
Kutokana na Jiji la Dodoma kukusanya zaidi mapato limesaidia kunyanyua makusanyo ya jumla ya mkoa huo, ambapo katika orodha ya mikoa umeshika nafasi ya pili baada ya kukusanya Tsh Bilioni 44.8 sawa na 56% ya lengo la Tsh. Bilioni 79.9 walizopanga.
Jafo amesema, Dar es Salaam ni kinara kwa mikoa kwa kukusanya Tsh Bilioni 77.03 kati ya TSh. Bilioni 174.4 inazotarajia kukusanya mwaka 2018/19.
Kwa upande wa manispaa, Iringa imekuwa kinara kwa kukusanya 64% wakati Manispaa ya Lindi ikishika mkia kwa kukusanya 20% ya malengo yake.
Kwa upande wa halmashauri, Geita mji imekuwa mbele ikiwa na 84% wakati Nanyamba inaburuza mkia kwa makundi yote kwani hadi Desemba ilikuwa imekusanya 9% pekee.
Wilaya ya Geita pia imeshika nafasi ya kwanza ikikusanya 78% ambazo ni TSh Bilioni 2.8 bilioni kati ya lengo la TSh Bilioni 3.6 bilioni.
Halmashauri za Nanyumbu, Msalala, Momba na Masasi zimeshika mkia kwa kukusanya chini ya 10% ya malengo.
Waziri Jafo amewataka Wakurugenzi wa halmashauri zilizokusanya mapato chini ya 20% wajitafakari kama wanatosha katika nafasi hizo.
Dar es Salaam imetajwa kuongoza kwa upande wa mikoa, Katavi umekuwa mkoa wa mwisho ukikusanya TSh Bilioni 2.4 sawa na asilimia 25 ya lengo la TSh. Bilioni 9.8 bilioni.
“Katika orodha hiyo tukiangalia wastani wa asilimia Dodoma inaongoza kwa asilimia 56 ikifuatiwa na Geita (53), Iringa (48) na mkoa wa mwisho utakuwa Mtwara (15), Katavi (25) na Kigoma wenye asilimia 27 ya makusanyo,” amesema Jafo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.