Oliver Mtukudzi, amefariki dunia Akiwa na Miaka 66

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia. Amefariki jana katika hospitali ya Avenues mjini Harare. Mtukudzi amekuwa akiugua kwa muda sasa.
Kwa mujibu wa BBC,Alilazimika kukatiza miadi kadhaa katika fani hiyo ya muziki katika mataifa mbali mbali duniani kutokana na kuugua kwake.

Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.
Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith.
Baada ya uhuru wa nchi hiyo, aliitumia sauti yake kuzungumzia masuala ya kisiasa na ya kijamii.
credit::bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.