kesi ya Wema ya kusambaza picha za ngono Upelelezi wake wakamilika

Mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu anatarajiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali kufuatia kukamilika kwa ushahidi upande wa Jamhuri juu ya kesi ya kusambaza picha za ngono inayomkabili.

Wema Sepetu anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo kupitia hatua hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.
Akiwa mahakamani hapo Mwanasheria wa Serikali,  Glori Mwenda amesema, “shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na taarifa njema ni kwamba upelelezi wa shauri hili umekamilika, hivyo tunaomba tarehe  kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali, mshtakiwa huyu
Wema anatetewa na wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa na katika kesi ya msingi anashtakiwa Oktoba 15, 2018 jijini Dar es Salaam alichapisha video ya ngono.
credit:Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.