Majaliwa amzungumzia Ruge

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema msiba  wa Ruge Mutahaba ni mkubwa kwa watanzania na serikali kwa sababu ametoa mchango mkubwa serikalini.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli mapema leo alipokuwa msibani, Mikocheni Jijini Dar es salaam, Majaliwa amesema Ruge amekuwa mtu wa  kutafsiri fursa za viongozi wa nchi kuanzia awamu ya nne na ya tano.
Majaliwa amesema Ruge alikuwa tayari kuwaongoza vijana kuwasaidia hata kwa kutumia fedha binafsi kuwafikisha kwenye matarajio yao.
"Jambo hili kwa serikali lilikuwa ni kubwa na ndio maana serikali imeendelea kushirikiana naye hata kwenye hili kwa sababu alisaidia vijana wetu kutambua umuhimu wa wao kuwa watanzania, umuhimu wa fursa tulizonazo kuzitumia vizuri na kwa wale walioshindwa kabisa kuwapa mwelekeo na wakati mwingine kuwashika mkono kuwapeleka mahali ambako panaweza kuwasaidia", amesema Majaliwa
Majaliwa amesema Ruge amewatumikia watanzania kwa kuzunguka nchi nzima kukutana na makundi mbalimbali ya watanzania kuwaeleza umuhimu wa kuitambua nchi yao hasa uzalendo na kutambua fursa zilizopo.
Mbali na Waziri Mkuu, Mbunge wa Iramba Maghararibi, Dkt Mwigulu Nchemba amesema kwamba, "Ruge hakuamini kwamba kuna muda unaoweza kukosa kazi kila muda ni kazi,".
Ruge Mutahaba alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, alifariki majira ya jioni huko nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figoa
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment