Majay Asema Alipofungua EFM Radio alimwambia Ruge anataka amuakuajiri, akacheka

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba bado anaumwa na tukio linaloendelea kwa sasa ni Watanzani na marafiki wa bosi huyo wanaombwa kuchangia gharama za matibabu ambazo mpaka sasa zimefika zaidi ya milioni 600.
Ruge ambaye ana mchango mkubwa kwa wasanii wengi, amelazwa nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa figo kwa kipindi kirefu.
Jumatano hii CEO wa EFM, ametua Clouds 360 na kufunguka mambo mbalimbali kuhusu mahusiano yake na Ruge ambaye amewatengeza vijana wengi kwenye tasnia ya burudani.
“Kabla sijafungua redio nilimwambia Ruge nataka kufungua redio akaniambia kwa sababu unaweza vitu vingi fungua, nilitaka kumfanyia surprise na nilivyofungua nikamwambia tayari nimefungua redio na nataka kufanya kazi na wewe yaani (Nimuajiri) akacheka sana kisha akaniambia acha mambo yako” alisema Majay.
Aliongeza, “Urafiki wetu na undugu wetu hauwezi kufa. Undugu, urafiki na ukaribu wetu hauwezi kufa kwa sababu ya kazi zetu kwani ukitaka kuwa mfanya biashara mzuri hutakiwi kuchukulia vitu personal kwenye kazi huwa tunafanya kazi, na ili ukae muda mrefu kwenye biashara hutakiwi kuchukulia vitu personal na ukichukulia personal lazima upotee” Majizzo
Mapema jana Mbaki Mutahaba ambaye ni ndugu za Ruge akielezea kiasi cha fedha ambacho kilitumika toka Ndg Ruge Mutahaba aanze kuumwa.
Unaweza kuendelea kutuma ujumbe wako wa faraja au kutuma chochote kupitia number 0752 222 210 na jina ni Kemilembe Mutahaba au kupitia CRDB Bank account number 0111055925300, 
Dr. Gelase Rwabyo Mutahaba.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment