Makonda Kumsaidia Msanii wa Injili Pascal Cassian

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amejitolea kumsaidia msanii wa nyimbo za injili Pascal Cassian ambaye amepasuka kibofu baada ya kupata ajali ya gari.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa 'Instagram' Makonda ameandika kuwa, "Pole sana ndugu yangu Pascal, nimefuatilia habari yako kwakweli imenisikitisha sana , tambua Mungu ni wetu sote, na Mungu huyu humpa jaribu mwanadamu, pia humpa njia ya kutokea kwa wakati wake wakati wa jaribu lako kutoka umefika, usiku huu nimekutafutia mlango wa kuondoa jaribu lako kwa kuzungumza na baadhi ya Madaktari wa Hospital yetu ya Muhimbili"
Ameendelea kuwa, "Nakuomba leo Februari 18, 2019 saa 5 asubuhi ufike Hospitali ya taifa Muhimbili,madaktari wetu watakuwa tayari kukupokea kukufanyia vipimo, nimewaelekeza watanipa taarifa tujue cha kufanya , amini kama tatizo nilakupatiwa ufumbuzi hapa basi tutafanya hivyo , na kama litahitaji kukupeleka nje ya nchi , basi niko tayari kusimama na wewe na kuhakikisha unapata matibabu nje ya nchi".
Pascal alipata ajali ya gari iliyopelekea kuvunjika nyonga na paja wakati akitoka kwenye mkutano wa injili mkoani Kigoma.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment