Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo asema haya alipofika Njombe

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ametinga mkoani Njombe na kufanya mkutano wa ndani na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe pamoja na vikosi maalumu vilivyopo mkoani humo kwa ajili ya kuchunguza matukio ya mauaji ya watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mabeyo amesema “vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi, na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,”
"Wananchi karibu nchi nzima wamesikia kinachoendelea Njombe, wengine yamewatia hofu lakini si Tanzania tu mpaka nje ya mipaka yetu taarifa zimesambaa,” amesema.
Kwa hiyo pasiwepo na hofu suala hili ni la kitaifa zaidi, linahusu pengine familia moja moja sababu zinajionesha kabisa ni za kifamilia zaidi,” amesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renatha Mzinga amesema watuhumiwa 30 wanashikiliwa kutokana na kuhusika kwao na utekaji na mauaji ya watoto hao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.