Ommy Dimpoz karudi nyumbani,Kasema Amezoea kuzuishiwa kifo


Karibu nyumbani ,Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amerejea nchini akitokea kwenye matibabu yake baada ya kuugua kwa muda mrefu alipokuwa amelezwa nje ya nchi.


Akizungumza katika uwanja wa ndege Jijini Dar es salaam alipokuw akirejea nchini Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.
Ommy Dimpoz amesema, "hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii."
"Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote." ameongeza Ommy Dimpoz.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.