Rais Magufuli ateua Wakurugenzi na Mwenyekiti

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Bw. Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund - PSSSF

Bw. Kashimba anachukua nafasi ya Bw.  Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine 2 kama ifuatavyo;
Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).
Na pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment