Ruge Mutahaba amefariki Dunia

Aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Cl;ouds Media Group Ltd, Ruge Mutahaba amefariki Dunia jioni ya leo Februari 26, 2019 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ruge alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Figo na Presha kwa zaidi ya miezi sita.
Kufuatia taarifa hizo, tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambi rambi.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment