Steve Nyerere Asema hamumombea mabaya Ommy Dimpoz

Msanii wa filamu Steve Nyerere amefunguka kumuomba radhi muimbaji Ommy Dimpoz kufuatia kauli yake mbaya “Ommy Dimpoz hataweza kuimba tena” aliyoitoa miezi michache iliyopita.

Kauli hiyo ilisambaa sana wiki hii baada ya muimbaji huyo kuachia wimbo ‘Ni wewe’ ambao unazungumzia machungu aliyoyapitia katika kipindi anaumwa.
Baada ya kauli hiyo kupingwa kwa nguvu zote na wadau wa sanaa pamoja na muimbaji mwenyewe, Jumamosi hii Steve ameibuka na kuomba radhi pamoja na kueleza nia yake.
“Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru M/Mungu, lakini pili nichukue fursa hii kumuomba radhi ndugu yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake. Na zaidi niwaombe radhi Watanzania wote na wapenzi wa sanaa.
Binadam unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea nami nakiri kukosea kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz.
Lakini ifahamike kwamba kauli ile haikuwa kwamba namtakia mabaya Dimpoz HAPANA, ila kwa tulivyokuwa tunapata taarifa kwakweli zilikuwa zinatukatisha tamaa.
Mengi yanaongelewa lakini mfahamu kwamba sikuwa na nia mbaya au nilikuwa na ugomvi na ndugu yangu huyu bali kama binadam hutokea kuteleza kwenye kuzungumza hivyo nawaomba suala hili lisichukuliwe kwa nia mbaya HAPANA.
Lakini tufahamu kwamba M/Mungu hufanya miujiza yake kutokana na sababu fulani, hivyo miujiza ya kumuinua ndugu yetu na kurudi kwenye kazi zake imetokana na imani aliyokuwa nayo Dimpoz kwa Muumba wake.
Najua mie niliteleza kusema kwamba Dimpoz hatoimba tena lakini sikuwa na nia hiyo, kwamba natamani Dimpoz asiimbe tena HAPANA. Hivyo pamoja na vichekesho mbalimbali vinavyotolewa juu yangu mie nafurahi sana kwani vinazidi kuupaisha wimbo mpya (NI WEWE) wa ndugu yangu na napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania na wapenzi wa mziki kumsupport ndugu yetu na kuzidi kumuombea dua kwa M/Mungu azidi kuimarika kiafya. AMIN🙏”
credit :Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment