Waandaaji wa SZIFF washambuliwa mitandaoni kisa ni tuzo ya muigizaji bora wa kike na kiume

Jana usiku kulikuwa na ugawaji wa tuzo za filamu za SZIFF, ambapo tulishuhudia waigizaji wa filamu wa ndani wakiibuka kidedea.

Ugawaji wa tuzo hizo, umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hususani kwenye kipengele cha muigizaji bora wa kike na kiume, ambapo washindi walikuwa ni Flora Kihombo na Rashid Msigala kupitia filamu yao ya KESHO.
Kiufupi hawa wote ni watoto na hata kazi yao haijapata kuonekana sana, ukilinganisha na filamu za waigizaji wengine kama Wema Sepetu, Monalisa, Gabo na wengineo waliokuwa wanashindana kwenye vipengele hivyo, jambo ambalo limezua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.

essau_esquireMsiandae tena hizi tuzo 🤧🤧🤧 na waigizaji msiendeshwe kisa Azam ndio wanaandaa hii SZIFF. Bora ujue hujaingia kwenye mashindano kuliko kuja kuburuzwa kama mlivyofanyiwa jana

pitwhizzy@___moh.d.r.t0_lee yan ndo maana Bongo hatuendelei asee umewahi kuona wapi watoto wanapambanishwa na wakongwe kwenye category moja walishindwa kuweka category ya upcoming au… Upumbavu huo

babranlaurentNimeshangaa sana Tuzo mwigizaji bora wakike anapewa huyo dogo badara ya wema nahuyo dogo apewe Tuzo ya msanii chipukizi wa wakike nalle Tuzo ya msanii bora wa kiume kapewa dogo wa kiume anaye alitakiwa apewe Gibo dogo apewe Tuzo ya msanii bora wa kiume anaye chipukia Azam tv mmepoteza sifa kwenye hili kanumba nae mmemkaushia hata Tuzo mungu Anawaona!

qutest_48 Yani labda km Azam mna Interest Zenu binafsi ila Mmeboa mnafanya watu Wajinga! @azamtvtz

qutest_48Yani mnaenda kuyazika haya mshindano kwa mikono yenu! UPUUZI MTUPU bora ning’oe dishi la Azam nifunge Star times mxiiiiiiiu yani ni MAZINGAOMBWE Kama Tuzo za Kilimanjaro @azamtvtz

hapixlucasmnaelekea kwny nyayo za kili awards tunawazika si muda

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment