Afadhali Ruge ametuachia watoto, asingekuwa na watoto tungeumia zaidi

Ikiwa ni siku mbili toka mazishi yapite ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa CloudsMedia, Ruge Mutahaba, Jumatano hii Mama mzazi wa marehemu amefunguka kuzungumzia mambo mbalimbali pamoja na kuwashukuru Watanzania kwa kumpatia heshima kubwa mtoto wake.

Akizungumza na mahojiano maalum na Clouds Media, Mama Ruge alisema mwanae huyo alikuwa anawapenda sana watoto wake na wao ndio kitu wanachojivunia kwa sasa.
“Ni wajuu wazuri, watakuwa Mungu atawasaidia, watasoma,” alisema Mama Ruge. “Afadhali ametuachia wajukuu, tunamshukuru Mungu. Angeondoka bila kuwa na mtoto tungeumia zaidi, lakini tunamshukuru Mungu ameacha watoto, watatufuta machozi,”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment