Binti Aliyezaa Mapacha wa Nne kwa Mpigo Aomba Msaada kwa Rais Magufuli

Binti wa miaka 24, RADHIA SOLOMONI Mkazi wa Mtaa wa Chemuchemu, Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam ambae amejifungua watoto wanne kwa mpigo, amemlilia Rais Dkt John Magufuli, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mawaziri na wote wanaogoswa kumsaidia mahitaji muhimu ya watoto hao kutokana na hali yake ya maisha kuwa ngumu na kushindwa kumudu mahitaji muhimu ya watoto wake.Akizungumza na Global TV Onlin, Radhia amesema, ujauzito wake ukiwa na mwezi mmojaalianza kuugua tumbo na kwenda katika Hospitali ya Mwananyamala, lakini baada ya kufanyiwa vipimo vya ultra sound, madaktari walimwambia kuna vitu hawavielei, hivyo wakamweleza kurudi baada ya wiki moja na walipompima akakuta ana ujauzito wa watoto wanne.Radhia anasema madaktari wa mwananyamala walimpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuanza kliniki kwani hawakuwa na uwezo wa kumsaidia kulingana na hali yake. Muda wa kujifungua ulipofika alijifungua salama watoto wanne ambao wawili ni wa kike na wawili ni wa kiume ambao wote ako hai na wanaendela vizuri.Atakaeguswa awasiliane nae kwa namba 0682 604 202 ili kumsaidia mahitaji ya watoto wake ikimo nguo, chakula, maziwa na mahitaji mengine madogo. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment