CCM,CHADEMA waongelea Maalim Kuhamia ACT WazalendoChama cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi uliofanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo umeonyesha na kuthibitisha kwamba utawala uliopo unaozingatia misingi ya Katiba ambayo CCM imeutekeleza.

CCM ilitoa kauli hiyo jana Jumatatu Machi 18, 2019 kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole   baada ya Maalim Seif kutangaza kuhamia ACT- Wazalendo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu yake kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.

“Huu ni Utawala wa sheria unaoruhusu mihimili ya dola kufanya kazi pasina kuingiliwa, watu wanazo haki kufanya uamuzi wa kisiasa kwa kujiunga na chama chochote.

“Hili ni fundisho kwa wale ambao wanasema mtu kujiunga na chama kingine maanake kanunuliwa, hii imedhihirisha ni uhuru wao wa kisiasa,” alisema Polepole 


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kilichotokea kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo ni sehemu ya mapambano.

Mbowe amesema hayo leo Jumatatu Machi 18 ikiwa ni muda mfupi kupita tangu Maalim Seif autangazie umma wa Watanzania kuwa yeye, viongozi na wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono wanahamia ACT- Wazalendo.

“Maalim na timu yake bado ni sehemu muhimu sana katika mapambano haya, tunawatakia kila la kheri,” amesema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nchini Tanzania.

Licha ya kuwatakia maisha mema huko ACT- Wazalendo lakini amewaomba wakafanye siasa kuanzia ngazi za chini ili kuhakikisha malengo ya kuwapigania wananchi yanafikiwa.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment