Irene Uwoya Kaamua Kuja na Products zinazomfanya awe mrembo

Baada ya mwigizaji Irene Uwoya kufungua bar yake siku kadhaa zilizopita sasa amekuja na bidhaa zake zenye brand yake kama lotion pamoja na kope kwaajili ya wadada ambapo lotion inafahamika kwa jina la “I Tone by Irene Uwoya”  na kope zinaitwa “I Lashes by Irene Uwoya”.

Irene Uwoya ameweka wazi kuhusiana na bidhaa zake kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa bidhaa hizo zitapatikana Tanzania nzima huku akihitaji support kubwa kutoka kwa Watanzania hii ni baada ya kuonyeshwa support kubwa kupitia kazi zake za uigizaji.

Huu mwaka nimeahidi na kuweka nia kubwa ya kuwa bega kwa bega na mashabiki zangu na wote wanaonifanya mimi kuwa Irene Uwoya...Na kwa mara nyingi sana nimekuwa nikipokea maombi na maswali nini hasa siri ya ngozi yangu inayovutia na kuwa nyororo na yenye kung’aa muda wote.Kwa kuwajali na kuwapenda sasa nimekuja na bidhaa ya I-tone by Irene Uwoya ikiwa ndio siri ya ngozi yangu na suluhisho la ngozi zenu ambayo haina madhara kwa ngozi za aina zote na hufanya kuwa na mwonekano wa mfano wa nuru ya jua mchana na nuru ya nyota usiku na yenye kuvutia...Nawapenda sana sana sana na kwa mara nyingine pia naomba support katika hili pia.Itapatikana Tanzania nzima na kwa wauzaji wa jumla punde ninatoa mawasiliano kwa ajili ya kuweza kuweka order kwa idadi yeyote utakayo...Naomba msiwe mbali sana na page yangu kwa ajili ya update.I-tone by Irene Uwoya...Solution for a flawless appearance.

Habari,Ukiniita Oprah hutakuwa umekosea ila kwa majina niliyopewa na wazazi wangu ni Irene Pankras Uwoya.Ni kwa muda mrefu nimeweza kufanya vingi na kufanikiwa katika sanaa yangu ya uigizaji na yote hii ni sababu ya support kubwa niipatayo kutoka kwenu mashabiki zangu na kiukweli nimebarikiwa kuwapata nyie katika maisha yangu...my fans are so loyal sababu kila ninalowaomba bila pingamizi mmekuwa zaidi ya msaada kwangu katika kuhakikisha lolote nifanyalo hamniachi peke yangu bali mnaniunga mkono kwa njia moja au tofauti.Mara nyingi ninapokuwa katika kazi zangu napenda sana urembo wa macho sababu naweza sema imekuwa silaha au kitu pendwa zaidi kwa mashabiki zangu pale ninapokuwa katika uigizaji au katika maisha yangu nje ya sanaa,na katika kuhakikisha wakipendacho mashabiki zangu nakiboresha basi mara kwa mara nimekuwa nikiweka urembo wa kope ambao unafanya macho yangu kuwa kivutio zaidi either niwe na make up au bila make up mara zote nimekuwa nikiweka kope tokana na kazi au mazingira husika kwa wakati huo.Hivyo basi kwa sasa nimekuja na biadhaa yangu ninayoitangaza leo kwenu iitwayo I-Lashes by Irene Uwoya ambayo itapatikana Tanzania nzima katika maduka ya urembo yote yaliyo karibu nawe na kwa kuanza kwa wauzaji wa jumla punde nitaweka mawasiliano kwa ajili na kuweza kuweka order kulingana na uhitaji wako.Kwa mara nyingine Naombeni sana support yenu bila kunichoka na nina wapenda sana sana sana.I-Lashes ni kope ambazo unaweza tumia zaidi ya mara 3 na zenye uhalisia ufananao na kope zetu halisi kwa size na model tofauti tofauti,usikae mbali na page yangu ili upate update zaidi.
I’m not perfect but my lashes are.....

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment