Jinsi Antu Mandoza kutoka Tanzania alivyonusurika kwenye ajali ya ndege ya shirika la Ethiopian Airlines

Mtanzania Antu mandoza ambaye ni Muigizaji, Mtangazaji na Mjasiriamali pia, amefunguka namna alivyonusurika kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliyotokea leo asubuhi majira ya saa 2.
Antu Mandoza kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa alitakiwa apande ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX ET302 lakini alibadilisha route na baadae akasikia taarifa za ajali ya ndege hiyo.
Antu anasema alipigiwa simu kibao kutoka kwa watu wake wa karibu wakimuulizia kama yupo hai, hii ni baada ya taarifa za ajli hiyo kusambaa mitandaoni.
I almost took the Ethiopian plane that crashed today I changed the route to Addis, I’m just landing and seeing the news and so many calls from the few people who knew I’m traveling with Ethiopia worried . God is good . Ningekua marehemu saivi🤭. Mungu mkubwa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment