Linah aongelea Kuhusu Kurudiana na Msanii mwenzake Amini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga, amefunguka juu ya tuhuma za kuvunja mahusiano yake ya kurudiana na Amini, jambo ambalo amesema halina ukweli wowote.

Akizungumza na www.eatv.tv, Lina amesema kwamba taarifa za yeye kurudiana na Amini hazina ukweli wowote, kwani wawili hao wamebaki kuwa marafiki tu, na sio wapenzi.
Akiendelea kufafanua hilo Linah amesema kwamba kamwe hawezi kurudiana na Amini, kwani hawezi kupasha kiporo, ila kinachoendelea kwao ni ushirikiano wa kikazi.

Afunguka zaidi

 

"Mimi na Amini hatujarudiana, ni marafiki wa kawaida tu, hakuna kitu kama hicho, ingekuwa hivyo ingeshaonekana, unajua mapenzi hayafichiki,hata kama ningekuwa namcheat, isingekuwa sehemu ambayo tayari nilikuwa na mahusiano naye, kwa sababu mimi nikienda nimeenda, huwa sipashagi viporo, tangu tulipoachana tumeachana”, amesema Linah.
Licha ya hayo Linah amekiri kuachana na baba mtoto wake, lakini Amini sio sababu ya yeye kuachana naye, isipokuwa walipishana kwenye masuala ambayo hawezi kuyaweka wazi, kwani ni ya kifamilia zaidi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment