Majonzi::RC Makonda, Gardner, AY na mastaa wengine wamlilia Kibonde

Kifo cha Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya Alhamisi hii mkoani Mwanza kimewashitua watu wengi kutokana na mtangazaji huyo kushiriki msiba wa aliyekuwa bosi wake, Ruge Mutahaba aliyezikwa Jumatatu hii huko Bukoba.
Baada ya Clouds Fm kutangaza kifo chake mastaa, viongozi na wadau mbalimbali wameanza kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia yake pamoja na kwa Clouds Media.
Hizi ni baadhi ya salamu zilizotolewa.
RC Makonda
Kifo Cha Kibonde kimeacha swali moja tu. Mahusiano yako na Mungu yakoje?. RIP Kibonde
AY
Nimestushwa sana na taarifa ya kifo chako Kaka yangu…Pumzika kwa Amani Kaka Yangu #EphraimKibonde…Tumeshirikiana kwenye Mengi ya Kikazi na Familia..Pumzika kwa Amani Wakukaja ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ.
Professor Jay
Hii ni SIRI yake Mungu aliye Hai na sisi Binadamu Hatujui SIKU wala SAA, 
Tuwaombee wapendwa wetu Watangulie salama na Wapumzike kwa Amani nasi Tunafuatia,
Pole sana kwa Familia za marehemu na ndugu zetu wa @cloudsfmtz @cloudstv
KAZI YAKE MOLA HAINA MAKOSA๐Ÿ™๐Ÿ™Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment