Mchungaji Alph Lukau aliyefufua mtu aomba radhi

Mchungaji Alph Lukau wa Afrika Kusini ambaye alitikisa dunia kwa habari ya kufufua mtu, ameomba radhi wananchi kwa kufanya tukio ambalo limekuwa msumari kwake.
Akizungmza na kituo cha redio cha Power FM cha Afrika Kusini, Mchungaji Lukau amesema kwamba mtu ambaye alionekana akimfufua, alikuwa hajafa kama ilivyosemwa, hivyo anaomba radhi kwa kutosema ukweli tangu awali.

Mchungaji Lukau ameendelea kusema kwamba mtu huyo alionekana kuwa hai kabla hajaletwa kanisani, na ndugu zake huenda walifanya hivyo wakiamini kuwa kuna kitu kinaweza kikatokea kwa ndugu yao ambaye alitangazwa kufariki.

Mwenyewe asimulia 

“Kabla ya kuingia maeneo ya kanisa, sanduku lilianza kutikisika, ikimaanisha kuwa mtu alikuwa hai. Samahani sana kwa uwasilishaji mbaya wa ukweli, mtu alikuwa hajafa na hajawahi hata kuwa mochwari kama ilivyosemwa awali, tulikuwa kwenye nyumba ya Mungu na mimi ni mchungaji tu, lakini samahani hatukuwaambia watu ukweli tangu mwanzo. Nadhani ndugu zake walimleta kanisani wakiamini kuna kitu kinaweza kutokea kwa ndugu yao”, amesema Lukau.
Akiendelea na mahojiano katika kituo hicho cha redio, Mchungaji Lukau amesema kwamba ingawa hakumfufua mtu huyo, alikiri kuwa alishawahi kurudisha uhai wa mtoto ambaye alifariki tumboni mwa mama yake, baada ya mapigo yake ya moyo kutoonekana, na mara baada ya maombi yalirudi.
“Mapigo ya moyo hayakuweza kupatikana, lakini baada ya maombi tukaambiwa mtoto yuko sawa”, amesema Alph Lukau.
Wakati huo huo mwanasheria wa kanisa la Alleluia Ministries International ambalo ni la mchungaji huyo, amekanusha taarifa za kulipa mtu aliyesadikiwa kufufuliwa, na kusema kwamba mtu huyo hakulipwa hata senti moja ili kushiriki muujiza huo.
credit::EATV
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment