MMhhhh Bonnah aweka wazi kuhusu kufumaniwa na mume wake

Mbunge wa Jimbo la Sergerea (CCM) Bonnah Kamoli, ameweka wazi kuwa hajawaji kufumaniwa na aliyekuwa mumewe kama jinsi watu wanavyozungumza na kusisitiza kuwa kama yupo mwenye ushahidi juu ya hilo autoe.

Bonnah amelazimika kujibu tuhuma hizo za ikiwa ni siku chache tangu akiri kuachana na mume wake, Mosses Kaluwa hali iliyomfanya yeye kubadilisha majina yae ya mwisho katika taarifa zake ikiwemo mitandao ya kijamii.
Tuhuma hizo za fumanizi zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakienda mbali na kusema kwamba sababu za kuachana na mume wake ni kutokana na kufumaniwa Jijini  Dodoma.
Katika Ukurasa wake wa Instagram Bonnah amesema kwamba, "wahenga wanasema jambo likiongelewa sana bila majibu linaweza kugeuka likawa kweli. Sasa ni hivi mimi Bonnah Ladisus Kamoli au jina langu lingine Neema sijawahi kufumaniwa hata siku moja katika maisha yangu".
"Sio kwamba mimi ni muadilifu sana au malaika ila hapakuwepo na mtu wa kunifumania nadhani mtakua mmenielewa na sitaongea tena na kama kuna mtu anaushahidi alete na kanifumania na nani", amemaliza katika maelezo yake.

Ujumbe wa Bonnah aliouweka katika ukurasa wake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment