Mrisho Mpoto Amjulisha Diamond Platnumz kuhusu msiba Ruge ‘amefariki Dunia njoo umzike’

Msanii wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto ameamua kumtumia ujumbe wa wazi msanii mwenzie, Diamond Platnumz kwa kumjulisha kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefariki Dunia.

Mrisho Mpoto kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa majonzi kwa kusema “@diamondplatnumz Nasib Abdul nimekwita jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia. RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE… Nimemaliza.”
Diamond Platnumz ambaye alishawahi kupitia kwenye mikono ya Ruge Mutahaba kipindi bado hajapata umaarufu, amekuwa kimya mpaka sasa aidha kuposti mitadaoni au kufika eneo la tukio la msiba huo kutoa pole.
credit::Bongo5
Hivi karibuni, Diamond aliingia kwenye bifu kali na Ruge Mutahaba kwa kutokubaliana kimaslahi kwenye ishu za kimuziki.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment