Mtangazaji PJ aingia Jahazini Kuziba pengo la Ephraim Kibonde

Clouds Media Group imemteua Mtangazaji Paul James (PJ) kuungana na Gardner G Habash pamoja na George Bantu katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM baada ya kuwepo pengo la mtangazaji tokea Ephraim Kibonde aliyefariki dunia March 7,2019.


Mtangazaji Paul James ambaye alikua kwenye kipindi cha Asubuhi  Power Break Fast sasa atatangaza rasmi kwenye kipindi hicho cha Jahazi ambacho hurushwa kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi mpaka saa moja jioni.

Paul James (PJ) aliwahi kuwa kati ya watangazaji wa mwanzo kabisa kutangaza kipindi cha Jahazi, alikuwa yeye na Gadner pamoja na marehemu Kibonde, baadae PJ alihamia kipindi cha Power Breakfast. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment