Poleni :: Wafanyakazi wa Clouds wapata ajali wakitokea Bukoba kuja Dar

Wafanyakazi wa 6 wa Clouds Media ambao walikuwa wakitokea Bukoba kwenye mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa CloudsMedia, Ruge Mutahaba kuja Dar es salaam wamepata ajali nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa walioitoa, wamedai mpaka sasa wafanyakazi hayo wamepelekwa hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Taarifa ya Clouds “Tunasikitika kuwataarifu kuwa sehemu ya timu yetu ya production (Watu 6) iliyokuwa ikitokea msibani Bukoba kurejea jijini Dar es Salaam imepata ajali ya gari maeneo ya nje kidogo ya Dodoma.
Tunamshukuru Mungu hakuna aliyepata madhara makubwa kutokana na ajali hiyo. .

Tunatoa shukrani za dhati kwa mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ndugu yetu Anthony Mavunde kwa msaada wa haraka aliowapatia vijana wetu ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu na vipimo zaidi Jijini Dodoma.”
credit:;Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment