Tanzia :: Ephraim Kibonde Afariki Dunia

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr.Thomas Rutachunzibwa, ametoa ripoti rasmi juu ya taarifa ya kifo cha mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde
Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, inasema kwamba Ephraim Kibonde alifia njiani akitokea hospitali ya Uhuru jijini Mwanza na kukimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando ilipo Mwanza.
Ikiendelea kueleza zaidi taarifa hiyo imesema kwamba Kibonde alianza kuumwa akiwa kwenye mazishi ya Ruge Mutahaba, na alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Kagera kwa matibabu, na kisha kupelekwa mkoani Mwanza, ili akapate matibabu zaidi.
Kibonde amefariki dunia Alfajiri ya Leo Machi 7, 2019, ikiwa zimepita siku 3 tu tangu Clouds Media Group wafanye mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba, aliyefariki Februari 26, 2019.


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment