Wezi Wavamia Wodi Ya Wagonjwa katika Hospitali ya Kilimanjaro na Kuiba Simu na Pesa


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah

Watu wawili wanaodaiwa kuwa vibaka, wamevamia kwenye wodi namba moja katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu.


Watu hao ambao inadaiwa walikuwa wawili, waliingia katika hospitali hiyo leo alfajiri Machi 25, 2019 majira ya saa 10:00 na kuiba vitu hivyo ambavyo ni mali za wagonjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai watu hao wawili ni vibaka.

Akizungumza shuhuda wa tukio hilo, Rebeca Msigiti ambaye alikuwa msaidizi wa mgonjwa katika wodi hiyo, amesema watu hao ambao ni wanaume, waliingia wawili ambapo mmoja alibaki mlangoni na mwingine akaingia ndani na kuchukua simu za wagonjwa na mikoba yao.

Amesema watu hao walipoingia wodini wao walidhani ni madaktari wameingia, kumsaidia mgonjwa ambaye alikuwa amezidiwa. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment