Zitto azungumzia Maalim Seif kugombea Urais 2020

Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka juu ya suala la nani atapewa ridhaa na chama kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akijibu swali la mwandishi lilohoji kuhusu habari zinazosemwa mitandaoni kuwa mwanachama mpya Maalim Seif ndiye atakuwa mgombea wa kiti hicho mwakani, ambapo alidai kuwa kwenye siasa siku moja ni kama mwaka mzima.
"Katika siasa hakuna mwanachama mgeni, kwani siku moja katika siasa ni kama mwaka mmoja", amesema Zitto.
Mapema Jumatatu ya Machi 18, 2019, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba, kufuatia mgogoro wa CUF uliodumu kwa zaidi ya miaka 3.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama, majira ya saa nane mchana Machi 18, 2019, Maalim Seif alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment