Hii ndo siri ya Maalim Seif Kuhama na Wanachama wa CUF

Makamu wa kwanza wa Rais (Mstaafu) wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuhamia kwake chama cha ACT Wazalendo hakijawachanganya wanachama wa CUF
.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema wanachama wa CUF walioamua kuhama naye tayari walikuwa wamechoka mgogoro ndani ya chama hicho.

"Kuhama kwangu sidhani kama tunavuruga wanachama wenyewe walishachoka na mgogoro huu, waliumia nilivyohama lakini baada ya masaa matatu tu baada ya kuhamia ACT-Wazalendo walifarijika na mliona walivyonifuata, tunashusha Tanga, tunapansisha Tanga" Maalim Seif Hamad," amesema.

Aliendelea kwa kusema, 'Hayakuwa ni maamuzi ya ghafla kuhamia ACT- Wazalendo tulijipanga baada ya kuona dalili ya kunyang'anywa chama, niliwaambia wenzangu wasiwe na shaka sisi ni washindi'. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment