Mh.Januari Makamba atangaza mwisho wa mifuko ya plastiki

Waziri wa Mazingira, Januari Makamba amesema mpaka kufikia Julai moja Tanzania itakuwa haitumii tena mifuko ya Plastiki ambayo inatajwa kuwa hatarishi kwenye mazingira.

Akijibu swali la Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya aliyeuliza ni lini Serikali itachukua hatua za haraka za kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ilhali Zanzibar, Kenya na kwingineko wameweza?
Makamba amesema kwamba ameelekezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kukutana na taasisi mbalimbali za Serikali, ikiwepo NEMC,TBS na nyinginezo zinazohusiana ili kuweka utaratibu maalumu wa kuweza kupiga marufuku ya matumizi ya plastiki.
"Kama tukakubalia katika vikao vya wiki hii na vinavyokuja basi Julai 1, inawezekana ikawa mwisho wa matumizi ya mifuko ya Plastic hapa nchini. Tumekaa na wadau wote na tumeona hakuna sababu yoyote ya kuendelea kutumia mifuko hiyo nchini. Mbadala upo na unawezekanaa mimi kama Waziri wa Mazingira nakubali hilo".
Hata hivyo amesema kwamba pindi serikali itakapopiga marufuku inapaswa kuwe na utaratibu maalumu ili zoezi  hili liweze kufanikiwa.
Sanjari na upigaji marufuku, Waziri Makamba amesema kwamba anaamini ajira nyingi zitatengenezwa kuliko zilizopo kwenye mifuko ya plastiki.
credit::eatv
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment