Msanii wa Muziki Jessie afariki dunia

Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka THT, Jessie, amefariki dunia. Jessie ni dada wa msanii, Jolie.

Mmoja kati ya wasanii kutoka THT, Mwasiti Almas ambaye amesema ni kweli kuwa msanii huyo amefariki dunia.
“THT imepoteza jembe leo Ooh Jessie mdogo wangu,umeenda na wewe…ALLAH akupumzishe salama ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ,” aliandika Mwasiti kupitia Instagram yake.
Hata hivyo Mwasiti hakuelezea chanzo cha kifo chake kutokana na kutokuwa sehemu rafiki kwaajili ya mazungumzo na kuahidi kuwa ataeleza taarifa zaidi.
Marehemu Jessie enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nyimbo ya ‘Mapenzi Kamali’ aliyomshirikisha Madee. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kifo chake kimetokea hospitali wakati wa kujifungua
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment