Ommy Dimpoz Kufunga Ndoa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz, ameshtua watu baada ya kumuomba msanii mwenzake Hamisa Mobetto amuoe.


Tukio hilo limejiri baada ya Ommy Dimpoz kupost picha instagram na Hamisa Mobetto kukoment, ndipo Ommy akatumia fursa hiyo kumuomba Hamisa amuoe, na kukubaliwa na mlimbwende huyo mwenye kibao cha 'my love' hewani.

Ommy Dimpoz hivi karibuni aliamua kufunguka kuhusu maisha yake ya mahusiano, baada ya watu wengi kujiuliza kama yuko kwenye mahusiano ama la, na kusema kwamba anatafuta mchumba ambaye atajua jinsi ya kumuhudumia ili amuoe rasmi, kwani hataki maisha ya kuishi na mwanamke bila ndoa.

Kutokana na post hiyo baadhi ya watu wametoa maoni kuwa wawili hao wanapendeza kuwa pamoja, hivyo sio jambo baya endapo wakiamua kuoana.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment