Rapper Nipsey Hussle, aliyepigwa risasi nje ya duka lake hadi kufa Los Angeles nchini Marekani

Wengi wakimjua kama Nipsey Hussle lakini jina lake la kuzaliwa likiwa ni Ermias Joseph Asghedom aliyezaliwa miaka 33 iliyopita August 15, 1985 kusini mwa Los Angeles nchini Marekani na kupoteza maisha yake March 31, 2019 (aged 33) Los Angeles, California, U.S.A ikiwa ni nje ya duka lake la nguo.
Baada ya kupoteza maisha Wasanii maarufu nchini Marekani wakiwemo Drake, Rihanna na J Cole wametoa rambi rambi zao kufuatia kifo cha rapa wa Los Angeles Nipsey Hussle, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mjini humo.
Msanii huyo wa miaka 33 alipigwa risasi nje ya duka lake la kuuza nguo.
Drake alimuelezea marehemu kama “mtu maarufu mwenye heshima”, huku Rehanna akiandika katika mtandao wake wa Twitter: “Hii haingii akilini, Nimeumizwa sana na tukio hili!”
Watu wengine wawili walijeruhiwa katika kisa hicho cha ufyatulianaji risasi kilichotokea nje ya duka la Marathon kusini mwa mji wa Los Angeles.
Luteni kanali Chris Ramierez wa kitengo cha polisi cha Los Angeles ameambia vyombo vya habari katika eneo la tukio kuwa mshukiwa aliyetekeleza uhalifu huo alionekana kama mwanamume mweusi.
Albamu ya kwanza ya msanii Nipsey Hussle, kwa jina ”Victory Lap” aliteuliwa kuwania albamu bora ya mwaka ya muziki wa rap katika tuzo ya Grammy.
Wasanii wengine ambao waliteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Cardi B, Mac Miller, Pusha T na Travis Scott.
CREDIT ::BONGO5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment