Wabunge wa Upinzani Watoka Nje Bungeni Kisa Lema

Wabunge wa upinzani wametoka nje ya kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma baada ya Kamati ya Maadili kusoma ripoti iliyotoa adhabu kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Kamati hiyo imemtia hatiani Mbunge huyo kwa kudharau Bunge kwa kuita Bunge ni dhaifu na hivyo kamati imeazimia Lema kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo.

Utakumbuka siku moja iliyopita wabunge wa upinzani walitoka nje tena mara baada ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naye kusimamishwa kuhudhuria mikutano miwili kwa kuunga mkono kauli ya CAG ya kusema mbunge ni dhaifu. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment