HABARI ZA MASTAA P Funk “Jina la Majani limetokana

Mtayarishaji mkongwe wa hits kibao na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records P Funk Majani amefanya mahojiano na  Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL leo May 2,2019 na ameweka  wazi kuhusiana na historia ya jina lake ‘Majani’.

Kutokana na P Funk Majani kuwepo kwenye industry ya muziki kwa muda mrefu ametaja list ya watayarishaji anaowakubali na amefunguka kuwa aliwahi kufanya album nne za Prof. Jay ikiwemo na Album za Juma Nature.
“Kwa sasa nipo bize sana, sishindi studio maana nimekaa studio kwa miaka 25 yani nimejifungia kwenye chumba kutengeneza beat, sasa hivi nimekuwa kama Kuku aliyetolewa bandani nipo huru”
“Jina la Majani limetokana na kipindi hicho natoka section studio so nikiwa naenda kwenye mgahawa kula nilikuwa naomba waniwekee mboga za majani nyingi ‘Weka Majani mengi’ kuanzia hapo ndiyo nikaanza kuitwa ‘Majani’ “
“Maproducer mara nyingi hatuangalii mistari ya msanii bali tunaangalia uwezo wa msanii huyo yaani sauti yake ipo vipi, maana sauti ni kama beat katika muziki.Niliweza kufanya album nne na @professorjaytz nimefanya album 4 na @sir_nature pamoja na baadhi ya ngoma ambazo zingine ni viporo nimefanya na @jaymoefamous “
“Producer ambaye namkubali kwenye Afro pop ni @abbah_process , kwenye Hip hop @cjamokertz , Kwenye Trap S2kizzy pia hata Mr 2touch ni Producer mzuri japo kuna wakati beat zake zinajiridia ila ni producer mzuri”
credit:millardayo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment