MKURUGENZI MKUU WA NEMC ATEMBELEA KIWANDA CHA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA AMBACHO KINAFANYA UZALISHAJI WA MIFUKO KWA MIAKA 10 SASA.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi, Dkt. Samuel Gwamaka ametembelea kiwanda kinachojishughulisha na uzalishaji wa mifuko mbadala ili kujionea kiasi cha uzalishaji na uhakika wa upatikanaji wa mifuko hiyo.

Dkt. Gwamaka alifurahia ufanyaji kazi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na watanzania, kwasababu asilimia 90 ya malighafi wanazotumia zinatoka hapahapa Tanzania. Vilevile tayari kimeajiri watu zaidi ya 25, na vibarua zaidi ya 45. Aliongeza kuwa kwasasa Serikali ipo tayari kuwasaidia wale wote ambao wanataka kujikita kwenye uzalishaji wa mifuko mbadala.Alimalizia kwakuwatoa wasiwasi wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala nakusema kuwa wananchi wafate sharia kwasababu katazo la mifuko ya plastiki ni kwaajili ya kulinda mazingira na afya zao pia.

Kwa upande wa waendeshaji wa kiwanda hicho, wamesema kuwa wamefurahia katazo la mifuko ya plastiki kwani wanaamini kutokana na mahitaji ya mifuko mbadala kuwa mingi watazidi kuongeza ajira kwa kinamama na vijana ukizingatia uzalishaji wa mifuko hiyo hauhitaji elimu kubwa ya darasani.
Dkt. Gwamaka akipatiwa maelezo na wahusiki wa kiwanda cha mifuko mbadala namna ambavyo wanaweza kutengeneza mifuko mbadala ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba vitu vyenye asili ya maji maji.


Dkt. Gwamaka akipewa maelezo na namna ambayo mashine zinavyofanya kazi.


Dkt. Gwamaka akipewa maelezo na namna ambayo mashine zinavyofanya kazi.


Share on Google Plus

About john

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment