Mwili wa kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi ambaye pia ni baba wa rais wa DR Congo, Felix, unatarajiwa kuwasili leo baada ya miaka miwili ya kifo chake

Mwili wa kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi ambaye pia ni baba wa sasa wa rais wa DR Congo, Felix, unatarajiwa kuwasili nchini humo leo baada ya miaka miwili baada ya kifo chake. Kulingana na familia, mwili huo utawasili kutoka nchini Ubelgiji kwa mazishi.
Kwa mujibu wa BBC. Alifariki mjini Brussels akiwa na umri wa miaka 84 mnamo mwezi februari 2017 lakini mwili wake ulisalia katika mji huo wa Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa kisiasa kwa utawala wa rais wa zamani wa taifa hilo Joseph Kabila.

Mazishi yake yatafanyika katika Viwanja vya Mashahidi, kulingana na nduguye Askofu Gerard Mulumba.
Mulumba anasema kuwa baada ya kuukaribisha mwili katika uwanja wa ndege , uatasafirishwa hadi katika uwanja huo kwa maombolezi .
Amesema kuwa tayari maandalizi katika uwanja huo ikiwezmo ujenzi wa jukwaa umekamilika mbali na yale ya maafisa wa polisi ambao wataongoza gwaride ili kumpatia heshima za mwisho baba huyo wa upinzani DRC.
Takriban marais watano wa bara la Afrika wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake.
CREDIT:BONGO5

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment