Ordha ya Maeneo ya Dar yaliyoathirika zaidi na mvua zinazoendelea kunyesha

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa tahadhari kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu athari za mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema taarifa ambazo anazo ni kwamba kuna watu 8 wamekufa kutokana na mvua hizo.Amefafanua taarifa rasmi itatolewa kwani kinachoendelea sasa ameagiza kata zote kufanya tathimini ya athari za mvua hizo.

Ameongeza vifo hivyo vimetokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameeleza ipo haja ya wakazi wa Jiji hilo kuhakikisha wanakuwa makini katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

"Mvua hizi zimesababisha maafa ambako taarifa ambazo ninazo kuna watu 8 wamefariki dunia kwasababu ya hizi mvua.Tutatoa taarifa rasmi baadae.Pia mvua zimesababisha kuharibika kwa miundombinu na barabara nyingi kutopitika,"amesema Makonda wakati anazungumzia athari za mvua akiwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salam ambako eneo hilo maji yamejaa.

Pia Makonda amesema athari za mvua hizo zingeweza kuwa kubwa zaidi iwapo watu wangetoka majumbani kwao, na hivyo ameshauri ni vema Walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakatoa ruhusa kwa siku mbili ili wanafunzi wasiende shule ili kuepuka maafa kwani baadhi ya magari yamekuwa yakitumbukia mtoni.

"Nito rai kwa walimu wakuu na hasa kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa taarifa walimu wa shule zote kuwa kwa siku mbili hizi yaani Jumanne na Jumatano wanafunzi wasiende shuleni.

"Hii itasaidia kupunguza maafa ambayo yanaweza kutokea kwa kuruhusu watoto waende shule huku tukijiua miundombini yetu haiko salama.Kwa wale ambao wako mabodeni nishauri waondoke huko kwani wanaweza kupata athari zaidi na kwamba hakuna sababu ya kupanda juu ya paa la nyumba kulinda bati,"amefafanua Makonda.

Makonda ameitumia siku ya leo kufanya ziara ya kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambako ameshuhudia namna ambavyo mvua hiyo imeleta madhara katika maeneo mbalimbali ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha hawajengi kwenye njia za maji na kubwa zaidi kutunza mazingira.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment