Tundu Lissu atangaza tarehe ya kurudi Tanzania

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ametangaza rasmi tarehe ya kurudi Tanzania baada ya kukaa nje ya nchi akifanyiwa matibabu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Akizungumza kwa njia ya simu kupitia na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika makao makuu ya chama hicho, Lissu amesema kuwa atarudi nchini tarehe 7 mwezi Septemba ikiwa ni miaka miwili tangu aliposhambuliwa.

Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo,” amesema Tundu Lissu.
Akiel;ezea kwanini amefanya maamuzi hayo ya kurudi siku aliyoshambuliwa, amesema kuwa amefanya hivyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.
Kuhusu mapokezi yake, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema mapokezi yake yatakuwa ya kitaifa.
Mhe. Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Jijini Dodoma mwaka 2017, na muda wote amekuwa akitibiwa nje ya nchi.


credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment