Nhlanhla Nciza wa kundi la Mafikizolo atangaza kuachana na mumewe

Nyota wa kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini Nhlanhla Nciza ametangaza kuachana rasmi na mume wake Thembinkosi “TK” Nciza aliyedumu nae kwenye ndoa kwa takribani miaka 15 mpaka sasa. Nhlanhla Nciza amepost taarifa hizo kupitia ukurasa wa instagram.

Nhlanhla na TK walibahatika kupata watoto watatu wa kiume ndani ya ndoa yao ambapo mwaka 2019 iliripotiwa kuwa mtoto wao wa kike alifariki dunia kwenye ajali ya gari. Nhlanhla ameshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa mume wake kipindi chote hicho na amesema kuwa watabaki kama marafiki wazuri kwa ajili ya watoto wao.
“Baada ya miaka 15 ndani ya ndoa yenye nguvu, mimi pamoja na  mume wangu TK Nciza tumekuja na maamuzi magumu kuhusu kuhitimisha mahusiano yetu, nashukuru kwa ushirikiano tuliopeana ndani ya miaka yote hiyo kwenye ukuzaji wa watoto wetu”
“Tutabaki kwenye mazingira yenye amani na kuendeleza kuwa washupavu na mean mzuri kwa watoto wote sisi kama wazazo, tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kutoka kwa marafiki na familia kwa ujumla” >>> aliandika Nhlanhla.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment