Mtandao wa Facebook waunda mfumo mpya kubaini matangazo bandia

Mfumo huo umekuja baada ya Martin Lewis, mwanzilishi wa tovuti ya Money Saving Expert, kushtakiwa baada ya jina na picha yake kutumika kwenye matangazo bandia kwenye ukurasa wa Facebook.

Facebook iliamua kuchangia kiasi cha pauni milioni 3 kwa ajili ya kutengeneza programu ya kupambana na wadanganyifu nchini Uingereza.

Taasisi ya kujitolea ya Citizens Advice imebuni laini ya simu ili iweze kuwasaidia watu wanapokutana na wadanganyigu mitandaoni-si tu kwa matangazo.


Namna ya kuficha mawasiliano yako kwenye WhatsApp

Mitandao ya kijamii yabadili muelekeo wa ushawishi

Kadiri siku zinavyosonga mbele vitendo vya kitapeli vinazidi kuongezeka, hivyo taasisi hiyo inatarajia kuwasaidia watu 20,000 mwaka wa kwanza wa huduma watakayoitoa, na kutahadharisha kuwa mtu yeyote anaweza kuingia kwenye mtego huu.

Citizens Advice imeainisha viashiria vitakavyojulisha kuwa matangazo ni bandia

Tangazo lisilo na uhalisia-au bidhaa iliyo na gharama ya chini kuliko inavyotarajiwa.
unapoambiwa ulipe haraka sana, au kwa njia isiyo ya kawaida-labda kwa huduma za kuhamisha fedha au kwa kutumia vocha.
Mtu kuwasiliana na wewe bila kutarajia.
kuulizwa kuhusu taarifa zako binafsi kama vile nywila (password) au pini.
tangazo lenye picha za watu maarufu .
Ndani ya Facebook, timu ya watu wenye ujuzi imeundwa kwa ajili ya kuchunguza matangazo yaliyoripotiwa kwa kutumia mfumo huu mpya
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.