Mwanamuziki Harmonize Amemzawadia Gari Mwanamuziki Mkongwe Q Chief.

Msanii kutoka lebo ya WCB, Harmonize amempa zawadi ya gari Toyota Porte mwanamuziki Q Chief.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Julai 22, 2019 Harmonize amesema ameguswa na maisha anayoishi Q Chief kwa sasa na kuona ana kila sababu ya kusaidiwa ikiwemo kuwa na usafiri.

Harmonize alisema hata leo alipokuwa akienda katika mkutano huo uliofanyika hoteli ya Hyatt Regency, alitumia usafiri wa bodaboda na kumuomba amlipie atakopofika jambo lilimuumiza moyo.

Msanii huyo mkali wa kibao cha Niteke, Never give up, alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Q.Chief amekuwa kati ya msanii aliyemvutia kuingia kwenye muziki na kueleza siyo yeye tu wapi na wasanii wengine wakubwa waliong'aa kupitia yeye.

"Leo mpaka unaona wasanii wanaendesha magari, wanamiliki majumba kutokana na muziki na moja ya watu waliowavutia na walikuwa wakicopy nyimbo zao ni pamoja na Q.Chief na mimi nilikuwa mmoja wapo niliyekuwa nikiandika hadi kwenye daftari," alisema Konde Boy.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.